Dar
es Salaam. Wakati kuna madai ya mpasuko wa uongozi, ukata mkubwa na
madeni kwenye klabu ya Simba, rais wa klabu hiyo Evance Aveva amesema
ajiuzulu, wanaotaka afanye hivyo wafuate taratibu.
Akizungumza na gazeti hili jana, Aveva alisema
kuwa kuna vyombo rasmi ambavyo vinafanya kazi ndani ya klabu hiyo
zikiwamo kamati za kisheria, kamati ya mashindano, kamati ya utendaji na
kwamba kama kuna tatizo wanachama wanajua taratibu za kufuata.
“Matokeo ya mpira ni hali ya mchezo, tumewapa
wachezaji kila kitu, hakuna mchezaji anayedai zaidi ya posho yao ya muda
ya mchezo wao na JKT Ruvu, Sh600,000 na kule Shinyanga viongozi wote
tulikwenda na kuna motisha walipewa, sasa kosa letu viongozi ni
lipi?”alihoji
“Mkutano mkuu wa wanachama upo pale pale,
utafanyika Machi Mosi, wanachama walio hai wajitokeze kwa wingi pale
Bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay, Dar es Salaam,”alisema.
Alieleza kuwa hakuna tofauti kati yake namakamu
wake, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ ambaye inadaiwa kamati ya utendaji ya
klabu hiyo imempiga marufuku kujihusisha na masuala ya timu.
Kumekuwa na madai kuwa Kaburu amezuiwa kwa kile
kwa kuwa amekuwa akimwingilia kocha (Goran) majukumu yake ikiwa ni
pamoja na kugawa wachezaji.
“Madai hayo Kaburu tulimuuliza akakataa, hatuna
ugomvi wowote naye, ni kiongozi mwenzetu na tunaelewana vizuri na muda
si mrefu nimetoka kuzungumza naye kwa simu, alichaguliwa na wanachama
kama mimi, hatujafikia hatua ya kusimamishana, viongozi wote tupo kitu
kimoja,”alisema.
Kwa upande wake, Kaburu hakupatikana jana kuzungumzia mgogoro wake na viongozi wenzake licha ya kutafutwa kwa muda mrefu.
0 comments:
Post a Comment