Warts inaweza kutokea kwenye mikono. Sehemu zilizoota vinundu ni vinyama vilivyoota na ukiviangalia kwa makini vinamwonekano kama taulo.  
Vinaweza kuota pia kwenye ulimi, mashavu ya uke, mapajani, katika lips za mdomo na usoni.
Vinyama hivyo pia vinaweza kutokea usoni, hasa sehemu karibu na kope ama maeneo mengine kama vile vidole vya miguu na mikono.
Madhara
Warts inaweza kubainika kwa vipimo vya maabara. Warts zikitokea katika shingo ya kizazi, inaelezwa kuwa inasababisha saratani ya kizazi kwa wanawake na kwa upande wa wanaume inasababisha kansa kwenye sehemu ya njia ya mkojo.
Anasema mtu wenye maambukizi ya virusi vya Ukimwi yupo katika hatari ya kupata ugonjwa huo kwa sababu nyama hizo huota na kukua kwa haraka kutokana na upungufu wa kinga iliyoshuka.
Matibabu
Dk Mushi anasema licha ya ugonjwa huo kusababisha madhara kwa binadamu, ikiwamo saratani na kukosa mtoto, lakini unatibika ikiwa mgonjwa atawahi matibabu.
Dk Mbasa ambaye pia ni specialist wa Magonjwa ya kifua kikuu na ukoma anasema tatizo la ugonjwa huo linaongezeka kila siku kutokana na uelewa mdogo kwa baadhi ya jamii.
Anasema baadhi ya wanaume walio katika ndoa ambao huomba kufanyiwa tohara katika hospitali hiyo, wengi wao wanakutwa na ugonjwa huo na kuanzishiwa matibabu.
Mikakati kuukabili
Dk Mbasa anasema moja kati ya mikakati inayoendelea kwa nchi nzima ni katika kupambana na ugonjwa huo ni kutoa elimu na kuhamasisha jamii kwenda katika vituo vya kutolea tiba kwa ajili ya uchunguzi na tiba sahihi.
“Vilevile tunaendesha kampeni za tohara kwa wanaume kwani wanaume wanaotahiriwa hupunguza uwezekano wakupata warts kwa asilimia 77 hadi 95, huku upande wa maambukizi ya VVU, mwanamume ambaye amefanyiwa tohara hupunguza uwezekano wa kupata VVU kwa asilimia 60,” anasema.
Kundi hatarini
Daktari bingwa wa magonjwa ya kuambukiza na yasiyoambukiza kutoka Kliniki ya MediCorps, Francis Makwabe anasema watu walio na umri kuanzia miaka 14 hadi 35 wapo katika hatari ya kupata ungojwa huo hususan wanawake waliovunja ungo na wale walikatika umri wa kuzaa.
Dk Makwabe anasema wenye mimba wapo katika hatari ya kupata sunzua kwa sababu mama mjamzito anakuwa na upungufu wa kinga ya mwili.
Vilevile, anasema wagonjwa wa kisukari wapo katika hatari ya kupata ugonjwa huo kutokana na kupungua kwa kinga ya mwili pamoja watu wanaotumia dawa kali. Kundi jingine lililopo katika hatari ya kupata warts, analitaja ni la wale wanaofanya mapenzi kwa njia ya mdomo, kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja na kufanya ngono kinyume cha maumbile.
Mbali na kundi hilo vilevile watoto wadogo wanaweza kuambukizwa ugonjwa huo kwa kufanyiwa vitendo vya ubakaji.
Dalili zake:
Moja kati ya dalili za ugonjwa huo ni kuwa na vinyama au vinyuzi nyuzi mithili ya taulo laini katika sehemu za siri ambapo mara nyingi huwasha wakati wa joto au unaponyoa nywele sehemu za siri.
   

Advertisement

0 comments:

 
Top