ni takribani miak 2015 sasa leo wakristu wanaanza safari ya kukumbuka mateso na safari ya ukombozi,inachukua siku 40 katika mfungo huu.
  tafakari yangu haswa ni jinsi ambavyo watu huichukulia kwaresma,kila mmoja ana utashi na weledi wake tofauti kuhusu kipindi hiki,ni aghalabu sana kwa mtu wa imani ya kikristo kusema hana weledi juu ya kwaresma,
     mara nyingi watu hudhani hiki ndicho kipindi pekee cha kutenda mema na kuishi maisha yenye usafi wa  moyo,la hasha,bali ni kipindi cha toba,unapaswa kuishi maisha mema ya kumcha mungu muda wowote,maana maandiko yanasema hujui siku wala saa.Hivyo basi ni budi kuishi na kujitaid kuwa watimilifu muda wowote.

 hivyo wito ni huu:"RARUA MOYO WAKO NA SIO MAVAZI YAKO,NIRUDIENI MIMI KWA MOYO WAKO WOTE"


Advertisement

0 comments:

 
Top