Awali ya yote nianze kwa kukusalimu msomaji wa makala hii,natumai u buheri mwenye siha njema.
       fimbo yangu leo inawaeleka watu wenye kufanya au kupanga na kuratibu mauaji ya wenzetu wenye ulemavu wa ngozi,kwa takriban miaka 10 sasa hili tatatizo limekuwa likishamiri katika jamii yetu,ni dhairi kuwa watendaji wa uovu huu ni ndugu,rafiki,au jamaa zetu,na kadhalika watendwa pia ni watu wa nasaba yetu pia,
     je hawa hawana haki,au tunu ya uzima?,la hasha ni wenzetu wanamahitaji kama mimi na wewe,ni binadamu kamili wenye utashi,kwa nini tuwatese,kwa nini hatuwalindi,au ni ile dhana ya "utajiri",la hasha,hakuna utajiri wa namna hiyo,napata kigugumizi sana kusema sababu kubwa ni ushirikina,embu msomaj wangu nawe unisaidie katika jamii unayoishi tukio hili la mauaji ya albino linasababishwa na nini haswa?
           Kumekuwa na radiamali tofauti toka mataifa ya ughaibuni,mashirika ya kimataifa na taasisi binafsi kukemea na kulaani matukio haya,Taifa limetiwa doa sana na kupoteza taswira ya dhana ya utu na kuonekana kuwa sasa si salama tena kwa wenzetu wenye ulemavu wa ngozi,kila uchwao matukio yanazidi kuongezeka,mauaji,ujambazi.
           Tafakari yangu inanipa hisia kali sana na kunifanya niseme ni ukosefu wa upendo na hofu ya Mungu.Ukiwa na upendo ni aghalabu kukiuka haki ya  msingi na kumpokonya binadamu mwezio haki na tunu ya uzima toka kwa mwenyezi mungu.Nani alieenemeka kwa dhuluma akaishi milele katika dhuluma,mwisho wa ubaya ni aibu na fedheha,mbaya kabisa matukio mengine mzazi mmojawapo anashiriki katika kufanikisha uovu huu,nitoe rai kwako mzazi mwenye mtoto mwenye ulemavu wa ngozi,ulemavu wa ngozi sio laana,au balaa ni tunu toka kwa mwenyez mungu kwani kunakusudio maalum ,hata kwa weledi wa biolojia imefafanuliwa,ni jambo linalohusu vinasaba,hivyo sio laana.
Rai yangu ni nini kifanyike,kwani tumekuwa na tabia ya kuokoa magoli yaliofungwa,mfano hadi sasa hakuna mikakati madhubuti ya kuwalinda ila tukio likitokea utasikia tutatoa zawadi ya milioni tatu kwa atakae toa taarifa zitakazosaidia kupatikana kwa waliohusika au mtendwa,duh!Kwa nini fedha hizo zisitumike kutambua familia zenye walemavu wa ngozi na kuboresha makazi yao,kujenga shule au kambi itakayowatunza wenzetu wenye ulemavu wa ngozi, huku kukiwa na ulinzi.
      Swali wewe umechukua hatua gani katika kudhibiti hali hii,unadhani unaweza,au bado tuna dhana eti ni jukumu la polisi,lashasha ni jukumu langu na lako ,chukua hatua sasa.Pengine utajiuliza nichukue hatua gani?ni swala mtambuka,jiulize mtaani kwangu yupo mlemavu wa ngozi,mazingira haya ni salama,pia mzazi wa mlemavu anamtizamo gani?
ni mengi sana ya kujiuliza na kisha kuchukua hatua,hata mashuleni ni vyema kukawa na mikakati madhubuti ya kuratibu mienendo na ratiba za wenye ulemavu wa ngozi mfano je akitoka shuleni anapita wapi,njia apitayo ni salama,au akiwa anaenda shuleni ni vitisho vipi vinamkabili.Naamini kuna matukio mengi ya ukatili wanayotendewa wenzetu ila hayaripotiwi katika vyombo vya dola,natoa wito kwa walimu wakiona kuna mwanafunzi mwenye ulemavu wa ngozi hajafika shuleni wafuatilie ili kujua nini kimemsibu na kutoa taarifa kwa mamlaka husika
Naomba kwa leo nifikie tamati kwa hapa.Ila naomba nikuache na swali.

Je nini kifanyike kutokomeza mauaji wa wenzetu wenye ulemavu wa ngozi?
            

Advertisement

0 comments:

 
Top