ikiwa yamebaki masaa machache kuelekea kuanza kwa bunge jipya la serikali ya awamu ya tano,mji wa dodoma umetawaliwa na sura za wageni,wengi wao wakiwa ni ndugu,rafiki na jamaa wa wabunge wapya waliochaguliwa kwa mara ya kwanza.
  Aidha tukio la kusisimua itakuwa ni zoezi la kuapishwa kwa wabunge hao wapya na uchaguzi wa spika wa bunge.Vyama mbalimbali vimeshapeleka majina wa wagombea wa nafasi hiyo kubwa ndani ya bunge kwa ajili ya uchaguzi.
kiuchumi ni hali njema kwa wamiliki wa nyumba za wageni mjini hapa kwani idadi kubwa ya wageni waliokuja hapa hulala katika nyumba hizo za wagen ambazo kwa sasa ni nadra kupata nafasi katika maeneo yaliyo karibu na mjini kwani yamejaa.
pichani ni baadhi ya wabunge wakiwa katika viwanja vya bunge kwa ajili ya kujisajili

Advertisement

0 comments:

 
Top