jaman kumbe udini umefikia hapa,yaani kuna mtu anapost vitu kwa kupingana na magazeti,mfano halisi ni juu ya Mh mbowe kukagua gwaride,yaan kuna mtu kaingiza hisia za udini,hivi kwani mtu huwezi baki na hisia zako za udini moyoni,au ukaangalia ni wapi pa kutamka,swala la mbowe kukagua gwaride na imani au lina uhusiano na dhehebu gani,mbona watu wengine wanakuwa wanatia nazi kwenye supu,
si dhani kama kuna dhehebu ambalo lina mamlaka dhidi ya jingine,au upendeleo fulani,
tuwe makini sana na matamko na nukuu zetu,tumia busara na uangalie hoja ambayo haina urari wa kiimani,maana sasa inatia shaka kuona misimamo ambayo haina tija,usijae hisia kuliko kutumia utashi na weledi.
TANBIHI:Ukiona mtu anasambaza jumbe zenye uchochezi wa kiiamani,tafadhali chukua jukumu la kumblock na kuifuta kabisa,pia mkemee na kumuelimisha

Advertisement

0 comments:

 
Top