Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama
Polycarp Kardinali Pengo amesema waumini hawana budi kusoma vizuri na
kuelewa Katiba Inayopendekezwa ili wakati ukifika, wafanye uamuzi kwa
hiari na utashi wao wakati wa kupiga Kura ya Maoni.
Ametoa kauli hiyo ikiwa ni siku mbili baada ya
Jukwaa la Wakristo kutoa tamko linalowataka waumini kujitokeza kwa wingi
kujiandikisha kwenye Daftari la Wapigakura, kushiriki kikamilifu kwenye
shughuli zote za elimu ya Katiba Inayopendekezwa na kupiga kura ya
“hapana” kuikataa Katiba Inayopendekezwa.
Lakini jana, Kardinali Pengo alisema kuisoma na
kuielewa katiba hiyo ndiyo wajibu wa msingi ambao Wakristo wanao kwa
sasa ili kupiga kura inayostahili wakati ukifika. Kuhusu maaskofu
kuagiza waumini waikatae Katiba Inayopendekezwa, Kardinali Pengo alisema
wao wakiwa viongozi wa watu, hawana mamlaka wala uwezo huo, bali wenye
uwezo ni wananchi wenyewe.
Hata hivyo, Kardinali Pengo alitaka tamko hilo
lisambazwe kwenye parokia na vigango vyote vya Jimbo Kuu la Dar es
Salaam ili waumini wasomewe, wauelewe kwanza, ili hatimaye waweze
kufanya uamuzi sahihi wakielewa ni nini wanachokitakiwa kukifanya.
Wito wa kardinali pengo ni kwa wananchi kuuosoma na kuuelewa waraka huo,kisha kufanya maamuzi stahiki
Wito wa kardinali pengo ni kwa wananchi kuuosoma na kuuelewa waraka huo,kisha kufanya maamuzi stahiki
0 comments:
Post a Comment