Ni wakati mwingine kwa Tanzania kujipanga katika soka baada ya
wiki hii Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kutangaza ratiba ya kufuzu kwa
fainali za Afrika mwaka 2017 (Afcon) na pia fainali za wachezaji wa ligi
za ndani (CHAN) za mwaka 2016, ambako Taifa Stars imepangiwa timu
ngumu.
Kama tulivyoonyesha wiki iliyopita kwamba safari
yetu ya kufuzu kwa mashindano hayo ni kama imemalizika hata kabla ya
timu yetu kugusa mpira, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wizara ya
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wanabeba jukumu zito ambalo ni kama
kupanda mlima mrefu ili kubadili matokeo.
Tunaliona ni jukumu zito kwa Stars kuzikabili
Misri, Nigeria na Chad ilizopangwa nazo Kundi G la mashindano ya Afcon,
ambayo mechi zake zinaanza miezi miwili ijayo.
Kwa upande wa CHAN, Stars inakutana na Uganda
Cranes, timu ambayo licha ya kutoka ukanda huu wa Afrika Mashariki na
Kati, lakini ina rekodi ya muda mrefu ya kuionea Stars kila
zinapokutana, iwe kwenye mashindano au mechi za kirafiki.
Mashindano ya CHAN yanayofanyika Rwanda, Januari
mwakani, tunaamini yangekuwa nafasi nzuri yetu kuwapa nafasi wachezaji
wetu, wakiwamo chipukizi ambao wamefanya vizuri kwenye Ligi Kuu inayokaribia ukingoni. 
0 comments:
Post a Comment