Moshi. Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi, Jaffar Michael
amefungua pazia kwa wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema), kutangaza nia ya kugombea Ubunge Moshi mjini.
Meya huyo alikwenda mbali zaidi na kukitaka Chama
Cha Mapinduzi (CCM), kujiandaa kisaikolojia kuwa chama cha upinzani,
kwani mwaka huu kitaangushwa kama alivyoangushwa Goodluck Jonathan wa
Nigeria.
Michael alitoa kauli hiyo mwishoni mwa juma katika
mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Kiusa mjini Moshi. Mkutano huo
ulikuwa na lengo la kufafanua masuala mbalimbali ya mji huo wa kitaifa
na kimataifa.
Baada ya kumaliza hotuba yake, meya huyo aliruhusu
maswali kutoka kwa wananchi na ndipo mkazi mmoja wa eneo hilo
alipomuuliza kama atakuwa tayari kugombea ubunge katika Jimbo la Moshi
Mjini. Swali hilo liliwafanya wananchi kulipuka kwa makofi na mmoja wao
alimtunza aliyeuliza swali hilo kwa Sh10,000.
Akijibu swali hilo, meya huyo alisema kama mbunge
wa sasa, Philemon Ndesamburo ataamua kupumzika, yeye atachukua fomu ya
kuwania ubunge na atasimama kama chama chake kitampendekeza.
Hata hivyo alisema, hata kama chama chake
hakitapendekeza jina lake, atakuwa tayari kumuunga mkono mgombea yeyote
atakayepitishwa na upinzani.
Kuhusu CCM kujiandaa kisaikolojia, Michael alisema
wapo Watanzania wana shaka kwamba Ukawa inaweza isiingie Ikulu na
kusema safari hii lazima ing’oke.
“CCM kianze kujiandaa kisaikolojia, alisema.
mwaka huu lazima king’oke,” alisemaa
, mwaka wa mwisho wa CCM kuongoza nchi hii ni
mwezi Novemba mwaka huu wa 2015. Mwezi huu Ukawa itaingia Ikulu na
kuizaa Tanzania upya,”alisema.
“Kila mmoja ajiandae na CCM wajiandae kisaikolojia
kuwa chama cha upinzani katika taifa hili. Watu wengi wanaamini kama
vile haiwezekani lakini hata Goliati alipopigwa na Daud hakuamini”
“Daudi na udogo wake na jeshi lake dogo alimpiga
Goliati. Kwa hiyo CCM ni Goliati aliyeoza kabisa ambaye tutamuondoa bila
yeye mwenyewe kuamini kama Jonathan alivyoondolewa Nigeria,”alisema
0 comments:
Post a Comment