Wanajeshi wa Cameroon, ambao wamekuwa kwenye mgomo baridi, kulalamikia kutolipwa mishahara yao, baada ya kuhudumu katika kikosi cha Umoja wa Mataifa, katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati, wamesitisha mgomo.Ripoti zinasema kuwa mgomo huo ulisitishwa baada ya serikali kuwalipa wanajeshi hao mishahara yao.
Wanajeshi hao walipiga kambi katika makao makuu ya jeshi mjini Yaunde hiyo jana wakitaka kulipwa mishahara yao.
Raia walizuiwa kutumia njia inayopita karibu na kambi hiyo ya jeshi wakati wa mgomo huo.Jeshi hilo limekuwa likihudumu nchini CAR chini ya wanajeshi wa Umoja wa Mataifa nchini humo maarufu kama MINUSCA, tangu kwa wa 2014.
Cameroonm ilituma wanajeshi 850 nchini humo na kila mmoja wao alikuwa akipokea mshahara ya dola elfu moja kila mwezi, lakini wengi wanadai kuwa walipokea nusu ya mshahara huo wakati huo wote.

0 comments:
Post a Comment