Msamaha ni mojawapo ya vipimo vya ukomavu, na ujasir. Mtu anaesamehe huwa anapata tiba ya moyoni. Msamaha hutibu jeraha la anaesamehe na kusamehewa. Msamaha husaidia kuboresha mahusiano.
Kuna kisa kimoja kiliwah kutokea, mkosaji alifanya Kosa hilo Kwa kusudi Huku akijua kuwa Hakuna atakachopoteza, Kwan mtendewaji hukuwa na uwezo wa kumfanya lolote, aidha Baada ya kufanya Hivyo, jamii nzima ilimlaan Kwa Kosa lile. Baada ya muda Alianza kupata ufaham kuwa jamii imemtenga, aliteseka sana kwani alikosa ushirikiano had Kwa ndugu zake. Alikata tamaa hadi kufikia hatua ya kutaka kujua. Kwa busara mkosewaji alimfuata na kumwambia nimekusamehe ,na kuitangazia jamii husika kuwa mgogoro wao umeisha. Ndipo jamii ikaanza kushirikiana Nae Tena. Kisa hiki kinaonesha jinsi gan Msamaha ulivyomponya mkoseaji

Advertisement

0 comments:

 
Top